Wapendwa wasomaji wa blogi hii mnakaribishwa nyote kufuatilia mada mbalimbali zitakazokuwa zikiandikwa zinazohusu lugha ya Kiswahili. Lengo ni kuchangia katika kukuza na kukuieneza Kiswahili nje na ndani ya Tanzania, barani Afrika na duniani kote kwa watu wenye hamu ya kutaka kujua na kuifahamu lugha hii adhimu ya Kiswahili.
Mada zitakuwa zinatolewa na walimu mbalimbali waliobobea katika somo la Lugha ya Kiswahili nje na ndani ya Tanzania. Maoni yako ni ya Muhimu sana katika kuboresha mada zetu juu ya somo la Kiswahili>
Mada hii ya dhana ya lugha ni mada muafaka kwa wale wote ambao wanahamu ya kujifunza lugha mbalimbali ulimwenguni. Mwanadamu hawezi kufanya jambo lolote pasipo lugha, ambayo ndiyo inayofanya watu wa mataifa mbalimbali wawasiliane.
Malengo ya mada hii mpya ya Lugha ni
1)kufahamu maana ya lugha kulingana na wataalamu mbalimbali
2)faida ya lugha
3)hasara ya lugha
KARIBUNI,
DHANA NA FASILI(MAANA) YA LUGHA
Wapo wataalamu mbalimbali waliojaribu kuifafanua maana ya lugha kwa mfano Mgullu(1999) katika kitabu chake cha Mtalaa wa Isimu akirejelea mawazo na maoni ya wataalamu mbalimbali amejaribu kuifafanua maana ya lugha kama ifuatavyo.
Trudgil,(1974)anasema "Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa kwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani yenye utamaduni wake"
Sapir,(1921) anasema "Lugha ni mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili autumie kuwasilishia mawazo, maoni na mahitaji. Mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari"
Weber,(1985) anasema "Lugha ni mfumo wa mawasiliano ya mwanadamu ambao hutumia mpangilio maalumu wa sauti kuunda vipashio vikubwa zaidi kwa mfano mofimu, maneno na sentensi"
Pia anadai kuwa lugha ni mfumo wowote wa mawasiliano ya watu kwa mfano lugha ya Kifaransa. lugha ya Kihindi.
Kamusi ya TUKI(1990)inasema,"Lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana"
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa lugha ni mfumo wa sauti za nasibu ambazo zimekubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika kukidhi mawasiliano yao ya kila siku katika nyanja mbalimbali za maisha mfano siasa, uchumi na utamaduni.
Kutokana na maana mbalimbali za wataalamu hao walionukuliwa na Mgullu(1999) tunapata mambo ya fuatayo yanayounda au yanayopatikana katika lugha yoyote ile kama;
a) lugha ni mfumo wa sauti. Sauti mbalimbali zinazopatikana katika lugha fulani hupangwa kwa namna ambayo sauti hizo huungana pale zinapotamkwa (au kuandikwa) kutoka sehemu mbalimbali katika mfumo wa utamkaji (utazungumziwa katika mada zijazo)
b) lugha ni sauti za mawasiliano: lengo kuu la lugha yoyote ni kukidhi mahitaji ya mwanadamu ambayo ni mawasiliano. Mawasiliano hayo husaidia katika kupanga,kuagiza na kutimiza mambo mbalimbali ya maisha ya kila siku ya mwanadamu.
c) lugha ni sauti za nasibu:Hakuna mwanadamu anayezaliwa akiwa anafahamu lugha bali hukutana nayo kibahati mbaya tu. Hujifunza tu pale anapowasiliana na watu au pale mtu anapozungumza na yeye kusikilza na kuiga mfano mtoto mdogo anapofikia umri wa kuanza kuongea hujifunza kutamka silabi au maneno macache taratibu mwishowe hutamka sentensi nzima. Vile vile dhana ya unasibu katika lugha ni kwamba hakuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kiashiria au kitaja(neno au jina) na kiashiriwa au kitajwa(kile kinachotajwa). Hakuna uhusiano kati ya neno meza na kitu chenyewe ambacho kinaitwa meza.
d) lugha ni sauti za nasibu za kusemwa na watu: binadamu ndiye kiumbe pekee mwenye kutumia lugha, wanyama ndege na viumbe wengine mfano wadudu wao hawana lugha hata kama wanatoa sauti mbalimbali zinazowawezeshs kuwasiliana. Kwa mfano Trudgil(1980) akinukuliwa na Mgullu(1999) anasema sauti za nasibu ambazo hutumika katika mawasiliano ni za wanadamu. Sauti hizi vilevile huweza kuwasilishwa kwa kutumia alama maalumu yaani maandishi ingaw pia chaweza kuwa kigezo dhaifu sana kubainisha unasibu wa lugha ya mwanadamu kwani alama hizo pia huashiria sauti za kusemwa na watu.
e) lugha kama chombo cha utamaduni fulani: kila lugha ina utamaduni wake. Lugha yoyote ile hutumikia utamaduni wa watu fulani hivyo basi hakuna lugha bora duniani kuliko lugha nyingine kwa mfano lugha ya Kiingereza si bora duniani kuliko Kichina , Kihispania, Kijerumani au Kiswahili hata kama Kiingereza kinatumika kila kona ya dunia hasa kwa shughuli za kimataifa ikiwa lugha hii ilisambazwa na Waingereza kipindi cha ukoloni sehemu mbalimbali duniani.
f) lugha ni njia ya mawasiliano: lugha yoyote ile lengo lake kuu ni kukidhi haja ya mawasiliano kati ya mtu na mtu au mtu na kundi au watu na watu. Hivyo kama lugha haikidhi mawasiliano haina maana.
FAIDA ZA LUGHA
Kulingana na maelezo hapo juu lugha ina faida nyingi kama ifuatavyo:
- Chombo cha mawasiliano miongoni mwa watu
- Chombo cha kukuza utamaduni wa jamii fulani kwani lugha yoyote lazima iwe na utamaduni wake kulingana na jamii ya watu husika mfano naman ya kutumia lugha kw akusalimiana
- Inaunganisha watu, lugha huunganisha watu wa jamii na mataifa mbalimbali kupitia ukalimani na utafsiri
- Kitambulisho
- lugha pia huweza kuwa kama kitambulisho cha utaifa au kabila mfano Mtanzania anayezungumza Kiswahili akiwa ughaibuni nje ya nchi yake na kukutana na mtu kutoka Tanzania anayejua kiswahili atafamika mapema pindi atakapozungumza.
- ]Lugha ina uwezo wa kukuza fasihi ya jamii husika iwe kwa njia ya maandishi au mazungumzo.
HASARA ZA LUGHA.
>Hasara kuu ya lugha ni utengano. Jamii huweza kutengana kwa kukosa mawasiliano pindi wakutanapo watu wasiofahamu lugh kila mmoja lugha ya mwenzake huwa kama bubu japo kwa muda mfupi.
MAREJELEO
Mgullu,R.S(1999)Mtalaa wa Isimu,Fonetiki,Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili, Nairobi Kenya, Longhorn Publishers(Ukurasa wa 6 hadi 10)
Wavuti wenu umenifaa kwani nasoma kiswahili mimi
ReplyDeletekama mwalimu mtarajiwa wa somo hili la kiswahili wafuti wenu utanifaa zaidi......
ReplyDeleteNashukuru kwa mchango wenu kukikuza kiswahili
ReplyDeleteNashukuru kwa mchango wenu kukikuza kiswahili
ReplyDeleteNashukuru sana kwa makala haya manake yameniwezesha kujibu maswali tulopewa na mhadhiri,mimi ni mwanafunzi wa Chou Kikuu Cha Eldoret,Kenya ninayefanya somo la Kiswahili na Jografia.Ahsante sana kutuelemisha na pia kutukuza kayika lugha yetu ya taifa.
ReplyDeleteSafi Sana inatusaidia kujifunza lugha sanifu.
ReplyDeleteAsnte sana nimejifunza mengi mimi ni mwanachuo kikuu cha dodoma tanzania
ReplyDeleteAsnte sana nimejifunza mengi mimi ni mwanachuo kikuu cha dodoma tanzania
ReplyDeletemko poa sana endeleeni kutusaidia lugha hii ya kizalendo ifike mbali.kiukweli mmekua msaaada sana kwangu kama mwanafunzi wakiswahili nchini Tanzania
ReplyDeleteSafi sana uko vizuri mwalimu nmeipenda hii tovuti lugha yetu ya kiswahili na kikue daima
ReplyDeleteHongereni kw kuzidi kkipa kiswahili nguvu kimatumizi
ReplyDeleteNashukuru Sana kwa fasili za kiswahili nilipo Soma hapo juu. Asante sana
ReplyDeleteNashukuru Sana kwa maneno haya, nimeshukuru
ReplyDeletekazi nzuri na muhimu kwa jamii zalishi
ReplyDeleteKazi kuntu! Japo mnafaa muwe na marejeo kadhaa ili kuipa kazi hii ubora wa kuridhisha.
ReplyDeleteKazi ipo vizuri.
ReplyDeleteAhsanten sana
ReplyDeleteSio wewe tu hata mimi pis
ReplyDeleteAsante nimeelewa
ReplyDeleteNtashukuru xna nimeelewa na imenisaidia Sanaa
ReplyDeleteNmeipenda, mmetoa wataalam hadi raha yani. Mbarikiwe
ReplyDeleteNzuri
ReplyDeleteMashaallah nimesoma mada hii shuleni haijaniingia ila hapa nimeipata na imeeniingia sana Alhamdulillah
ReplyDeleteNimepata kujua na wataalamu wengi Mashaallah
Ahsanteni sana
nzuri sanaaa
ReplyDeleteAhsanteni sana kwa huduma yenu nzuri kwetu sisi waalimu watarajiwa wa somo la kiswahili... Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma Tz.
ReplyDeleteNashukuru kwa makala hii.Nimejifunza kitu.
ReplyDeleteKazi nzuri.
ReplyDeleteInapendeza kazi nzuri
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteDaaaaaaaaaah sjawahi ona Kama hiii nimeipenda hiii nzurii
ReplyDeleteMarejeleo yafaa zaidi
ReplyDeleteNaelewa kuwa lugha ina faida nyingi kuliko hasara
ReplyDeleteKwanza kabisa ningependa kutoa shukurani zangu toka moyoni,nina furaha kwa kupata makala haha..nimeyasoma na nikaelewa maana ya lugha,sifa bainifu,faida na hasara za lugha,Asante I..ila kwa maoni yangu lugha haichangii Sana katika kuleta utengano baina ya watu wasofahamu lugha moja kwa sababu pia Kuna matumizi ya ishara Kama njia ya mawasiliano. Shukurani,,
ReplyDeleteAsanteniiii
ReplyDeleteAsanti Sana kwa tovuti hii..nimejifunza mengi
ReplyDeleteNashukuru sana kwa mchango mzuri.endeleeni na moyo huo
ReplyDeleteNmefurahia kazi yko
ReplyDeleteInaelezea vzur kiswahl inatusaidia kuelewa vzur tunakushukuru sana
ReplyDeleteAsanten xana
ReplyDeleteMm Richard mwakagali mwanafunzi wa kidato cha tano ruvuma mbinga agustivo high school .asante kwa mchangoo huu mkubwa
ReplyDeleteUchambuzi umeenda vizuri sana na umefahamika vyema
ReplyDelete